Tebboune: Jeshi la Algeria Liko Tayari Kujenga Hospitali Gaza na Kuwasaidia Wapalestina

Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune, ametangaza kuwa jeshi la nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika liko tayari kuingia Gaza kujenga hospitali tatu ndani ya siku 20 mara tu mpaka na Misri utakapofunguliwa.



Akizungumza Jumapili wakati wa mkutano wa kampeni, Tebboune aliahidi pia kupeleka mamia ya madaktari katika eneo la Palestina lililoharibiwa na vita na “kusaidia kujenga upya yale ambayo Wazayuni wameyaharibu.”

Tebboune, ambaye anawania muhula wa pili wa urais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 7 Septemba, alikuwa akihutubia wafuasi wake katika jiji la Constantine.

“Palestina si suala la Wapalestina pekee, ni suala letu pia,” Tebboune aliwaambia umati wa watu.
#freepalestine #palestinetanzania @middleeasteye

Post a Comment

0 Comments