ISRAEL YAKATA MAWASILIANO GAZA KUFICHA UKATILI WANAOUFANYA USIFAHAMIKE


Tarehe 28 Oktoba 2023, shirika la kutetea haki za binadamu " Human Right Watch," limetoa onyo kupitia tovuti yake rasmi, likisema kwamba kuvurugika kwa mawasiliano na mtandao katika Ukanda wa Gaza, ambao unakumbwa na mashambulizi makali ya Israel, kunaweza kutumika kama "kinga ya uhalifu na manyanyaso ya halaiki ."

Deborah Brown, mwakilishi wa shirika hili la kimataifa, alisema katika taarifa iliyotolewa leo Jumamosi kwamba kufungwa kwa habari kunaweza kuwa "kinga ya uhalifu wa kikundi na kuchangia kuepuka kuwajibishwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu kwa waliohusika kuua mifumo ya mawasiliano."

Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu Amnesty International, kwa upande mwingine, limeonyesha wasiwasi juu ya kupoteza mawasiliano na wafanyakazi wake huko Gaza na limegusia kwamba kuzimwa kwa mawasiliano kutafanya iwe ngumu zaidi kupata habari muhimu na ushahidi unaohusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita dhidi ya raia wa Palestina huko Gaza, pamoja na kusikiliza moja kwa moja wale wanaosumbuliwa na ukiukwaji huu.

"Net Blocks," huduma inayosimamia uunganisho wa mtandao, limetoa taarifa ya kuvurugika kwa mawasiliano katika Ukanda wa Gaza.

Kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Ushirikiano wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA), mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa yamepoteza mawasiliano na watumishi wenzao huko Gaza.

Msimamizi wa Masuala ya Kibinadamu wa OCHA, Lynn Hastings, amesisitiza kuwa shughuli za kibinadamu na shughuli za hospitali kamwe haziwezi kuendelea bila ya kuwa na mawasiliano."

Taasisi inayohusika na kutoa huduma za dharula kama za Afya THE PALESTINIAN RED CRESCENT limetangaza kwenye X (twitter) kwamba wamepoteza mawasiliano na kituo chao cha operesheni na timu zake zote huko Ukanda wa Gaza kutokana na kuvurugika kwa mawasiliano ya simu za mkononi, mtandao na mamlaka ya Israeli. Kuvurugika huku kunawaathiri kutoa huduma za dharura kwa namba 101 na kuzuia ufikiaji wa magari ya wagonjwa kwa majeruhi wanaohitaji msaada kutokana na kushambuliwa na Israel huku wakionyesha wasiwasi mkubwa juu ya uwezo wa madaktari kuendelea kutoa huduma chini ya hali hii, pamoja na usalama wa wafanyakazi wake.

Post a Comment

0 Comments