WAZIRI AOMBA SERIKALI YA SPAIN KUVUNJA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA NA ISRAEL


Waziri wa masuala ya Haki za Kijamii wa Hispania ameiomba serikali isimamishe uhusiano wa kidiplomasia na Israel kutokana na mauaji ya kupangwa dhidi ya watu wa Palestina.

Bi Ione Belarra amezungumza hayo katika mkutano wa ngazi ya juu uliofanyika mjini Madrid Spain ikiwa kama sehemu ya umoja wa nchi za ulaya 

"Leo, nimeomba mshirika wetu (katika serikali), Chama cha Kisoshalisti (PSOE), kwamba tuchukue suala hili kwa uzito zaidi katika mapambano dhidi ya mauaji ya kupangwa, yanayotekelezwa na Israel dhidi ya watu wa Palestina. Naamini kwamba tunapaswa haraka kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi ya Israel," Belarra alisema kwa waandishi wa habari.

"Pia, tunapaswa kuchochea mjadala katika ngazi ya Ulaya ili kutumia vikwazo vya kiuchumi kama mfano dhidi ya wale wanaotajwa kuwa wana jukumu la kisiasa katika mauaji haya," aliongeza.

Watu wasiopungua 471 waliuawa na wengine 342 kujeruhiwa katika shambulio la anga la Israel kwenye Hospitali ya Al-Ahli Baptist huko Gaza siku ya Jumanne usiku, kulingana na Wizara ya Afya huko Gaza. Hata hivyo, Israel imekanusha kuhusika na shambulio hilo.

Gaza tayari inakabiliwa na manyanyaso kama kukatiwa umeme, maji, chakula, mafuta, na vifaa vya matibabu vikiwa vinapungua."

Post a Comment

0 Comments