Misheni za kidiplomasia zilizopo Jerusalem na Ramallah zinazohusishwa na Umoja wa Ulaya (EU) zimesema kuwa uvamizi wa nguvu uliofanywa na Israel katika ofisi za UNRWA zilizoko Jerusalem ya Mashariki ambao ulihusisha kuchukua mali, kukata mawasiliano, na kushusha bendera ya Umoja wa Mataifa na kuiweka bendera ya Israel ni ukiukaji wazi wa Mkataba wa Haki na Kinga za Umoja wa Mataifa.
Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na misheni za EU huko Jerusalem na Ramallah, pamoja na nchi za Ufaransa, Ujerumani, Finland, Denmark, Uholanzi, Lithuania, Poland, Slovenia, Ugiriki, Cyprus, Austria, Uswidi, Uswisi, Ubelgiji, Ireland, Ureno na Hispania, zilitahadharisha kuwa hatua kama hizo zinaunda mfano hatari unaoonyesha kupuuzwa kwa sheria za kimataifa. Hii ni pamoja na Mikataba ya Geneva, ambayo inalinda mashirika yanayotekeleza majukumu muhimu ya kibinadamu kulingana na sheria za kimataifa.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa Israel inapaswa kuheshimu wajibu wake chini ya Mkataba wa Haki na Kinga za Umoja wa Mataifa, ambao unatoa ulinzi maalum kwa ofisi na mali za Umoja wa Mataifa na kuzuia uvunjaji wake kwa namna yoyote ile.
..........................
EU DIPLOMATIC MISSIONS SAY FORCIBLE RAID ON UNRWA PREMISES IN EAST JERUSALEM VIOLATES UN PRIVILEGES AND IMMUNITIES CONVENTION JERUSALEM
Diplomatic missions in Jerusalem and Ramallah affiliated with the European Union said that the forcible Israeli raid on UNRWA premises in East Jerusalem, which was accompanied by the seizure of property, the cutting of communications, and the replacement of the United Nations flag with the Israeli flag, constitutes a flagrant violation of the Convention on the Privileges and Immunities of the United Nations.
The joint statement issued by the diplomatic missions in Jerusalem and Ramallah affiliated with the European Union and the countries of France, Germany, Finland, Denmark, the Netherlands, Lithuania, Poland, Slovenia, Greece, Cyprus, Austria, Sweden, Switzerland, Belgium, Ireland, Portugal, and Spain said that such measures create a dangerous precedent for a complete disregard of international law, including the Geneva Conventions, which grant legal protection to organizations that carry out vital tasks in accordance with international humanitarian law.
It added that Israel must meet its obligations under the Convention on the Privileges and Immunities of the United Nations, which guarantees the inviolability of United Nations premises and prohibits their violation
T.R.

0 Comments