Wizara ya Mambo ya Nje na Raia waishio nje ya Nchi ya Palestina, inalaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea jijini Sydney nchini Australia, shambulio ambalo limesababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia na kuwaacha wengine wakiwa wamejeruhiwa.
Wizara inaeleza mshikamano wa dhati wa Nchi ya Palestina na Serikali ya Australia pamoja na wananchi wake katika kipindi hiki kigumu, na inasisitiza msimamo wake thabiti wa kupinga aina zote za vurugu, ugaidi na misimamo mikali.
Aidha, Wizara inatoa pole za dhati kwa familia za waathirika wa tukio hili la kusikitisha, na inawatakia uponaji wa haraka wale wote waliojeruhiwa.
.........
The Ministry of Foreign Affairs and Expatriates of the State of Palestine strongly condemns the terrorist attack that took place in Sydney, Australia, which resulted in the loss of life and left a number of people injured.
The Ministry expresses the State of Palestine’s full solidarity with Australia, its government, and its people during this difficult time, and reiterates its firm rejection of all forms of violence, terrorism, and extremism.
The Ministry extends its deepest condolences to the families of the victims and wishes a swift and full recovery to those injured.
0 Comments