Walowezi wa Kiyahudi wamechoma moto kibanda cha kilimo na miti ya mizeituni katika kijiji cha Dhahr Al-Abed.

Walowezi wa Kiyahudi wamechoma moto kibanda cha kilimo na miti ya mizeituni katika kijiji cha Dhahr Al-Abed, magharibi mwa Jenin katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu (West Bank), kulingana taarifa ya vyanzo vya ndani.

Mwenyekiti wa baraza la kijiji cha Dhahr Al-Abed, Tareq Amarna, aliiambia WAFA kwamba walowezi kutoka kituo cha ukoloni kilicho karibu na mashariki mwa kijiji walishambulia na kuchoma kibanda cha kilimo kinachomilikiwa na Nidal Amarna, mkazi wa eneo hilo. Moto pia ulichoma baadhi ya miti ya mizeituni.

Aliongeza kuwa walowezi, chini ya ulinzi wa jeshi la Israeli, waliwatisha wakulima na kutaka kuchukua mamia ya dunumu (ekari) za ardhi katika eneo la mashariki la kijiji cha Dhahr Al-Abed. Waliweka alama kwenye ardhi hizo kwa maandalizi ya kuzikamata, akisisitiza kuwa ardhi zote ni mali ya wakazi wa kijiji na zina hati za umiliki zinazothibitisha umiliki wao.

Amarna alieleza kwamba walowezi mara kwa mara hushiriki katika shughuli za uharibifu kwenye ardhi za kilimo zinazomilikiwa na wananchi, kwa nia ya kuzichukua kwa ajili ya upanuzi wa makoloni.

Post a Comment

0 Comments