Wafanyakazi wa UNRWA wafungua tena kituo cha matibabu kilichoharibiwa na mashambulizi ya Israeli mwezi Januari



Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limesema wafanyakazi wake huko Khan Yunis wamefanikiwa kufungua tena kituo cha afya cha UNRWA baada ya kuharibiwa vibaya mwezi Januari na mashambulizi ya Israeli.

"Kwakuwa hakuna vituo vingine vya afya katika sehemu hii ya Khan Yunis, kliniki hii ni muhimu sana kusaidia familia zilizohamishwa ambazo zimerudi eneo hili kutafuta makazi," ilisema UNRWA katika chapisho kwenye mtandao wa X.

Vikosi vya uvamizi vya Israeli vimeendelea na mashambulizi katika Ukanda wa Gaza, kwa nchi kavu, baharini na angani, tangu Oktoba 7, 2023, na kusababisha vifo vya zaidi ya raia 38,193, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na kujeruhi zaidi wengine 87,903.

Maelfu ya wahanga bado wamenaswa chini ya vifusi au wametawanyika mitaani.

T.R.

Post a Comment

0 Comments