Kufungwa kwa Msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa na mamlaka za utawala wa uvamizi wa Israeli ni ukiukaji mkubwa wa haki za watu wetu na ni uvunjaji wa haki ya hali iliyopo ya kihistoria na kisheria (status quo).
![]() |
| Mandhari ya Picha yanayoakisi hali ya ukimya katika Msikiti mtakatifuwa Al - Aqsa, si kawaida kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan |
Wizara ya Mambo ya Nje na Wahamiaji wa Kipalestina, inaeleza kulaani vikali mashambulizi yanayoendelea ya mamlaka za uvamizi wa Israeli dhidi ya Msikiti mtukufu wa Al-Aqsa, ikiwa ni pamoja na kuufunga kwa kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya waumini na kuweka vizuizi vikali vya kuingia katika Mji wa Kale na katika maeneo ya ibada huko Jerusalem kwa visingizio vya kiusalama, hasa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan.
Wizara inathibitisha kwamba Israel haina mamlaka ya kiserikali juu ya mji uliokaliwa kwa mabavu wa Jerusalem, wala juu ya sehemu yoyote ya ardhi ya Taifa la Palestina. Inasisitiza kwamba sera, vitendo na hatua za Israeli ni ukiukaji wa wazi wa haki za watu wa Palestina na ni uvunjaji dhahiri wa sheria za kimataifa pamoja na hali iliyopo ya kihistoria na kisheria ya maeneo matakatifu, ambayo lazima yalindwe. Hatua hizi pia zinawakilisha ukiukaji wa uhuru wa kuabudu.
Dola ya Palestina pia inasisitiza kwamba eneo la Al-Haram Al-Sharif / Msikiti wa Al-Aqsa kwa ukamilifu wake, lenye ukubwa wa dunamu 144, ni mahali pa ibada ya Waislamu pekee, na kwamba hatua zozote za upande mmoja zinazochukuliwa na uvamizi wa Israeli ni shambulio dhidi ya haki hii ya kihistoria na ya kisheria.
Wizara inaishikilia serikali ya uvamizi wa Israeli kuwajibika kikamilifu kwa ukiukaji huu na inaitaka kufungua mara moja milango ya Msikiti wa Al-Aqsa na kuondoa vizuizi vyote vilivyowekwa kwa waumini kuingia. Pia inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na taasisi zake zote kuchukua hatua za haraka kusitisha ukiukaji huu na kuhakikisha uhuru wa kuabudu katika Jerusalem iliyokaliwa kwa mabavu, ikirudia msimamo wake wa muda mrefu kwamba uvamizi lazima ukomeshwe na uwajibishwe mara moja.
.............
The closure of Al-Aqsa Mosque by Israeli occupation authorities is a serious violation of our people’s rights and an infringement of the historical and legal status quo
The Ministry of Foreign Affairs and Expatriates strongly condemns the continued assault by the Israeli occupation authorities on the blessed Al-Aqsa Mosque, including its closure by military force to worshippers and the imposition of strict restrictions on access to the Old City and places of worship in Jerusalem under security pretexts, particularly during the holy month of Ramadan.
The Ministry affirms that Israel has no sovereignty over the occupied city of Jerusalem, nor over any part of the land of the State of Palestine. It stresses that Israeli policies, practices, and measures constitute a blatant violation of the rights of the Palestinian people and a clear breach of international law and of the existing legal and historical status quo of the holy sites, which must be protected. These actions also represent a violation of freedom of worship.
The State of Palestine further emphasizes that the Al-Haram Al-Sharif / Al-Aqsa Mosque compound, in its entirety, covering an area of 144 dunams, is an exclusively Muslim place of worship, and that any unilateral measures taken by the Israeli occupation constitute an attack on this historical and legal right.
The Ministry holds the Israeli occupation government fully responsible for these violations and calls on it to immediately reopen the gates of Al-Aqsa Mosque and lift all restrictions imposed on worshippers’ access. It also calls upon the international community and all its institutions to take urgent action to stop these violations and ensure freedom of worship in occupied Jerusalem, reiterating its longstanding demand that the occupation must be ended and held accountable immediately.
#palestinetanzania #palestinatanzania

0 Comments