Ubalozi wa Palestina nchini Tanzania umeongoza maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, yaliyohudhuriwa na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, wanachama wa Kamati ya Mshikamano, wanajamii wa Kipalestina, pamoja na wageni mbalimbali waalikwa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Balozi wa Palestina, Bwana Salim Siam, alisema kuwa tangu kupitishwa kwa Azimio la Umoja wa Mataifa Na. 181 mwaka 1947, haki za Wapalestina zimeendelea kukiukwa, huku Taifa la Palestina likinyimwa haki yake ya msingi ya kuwa na dola huru yenye Jerusalem kama mji mkuu wake, sambamba na kuendelea kwa ukaliaji wa kikatili wa Israel.
Bwana Siam alieleza kuwa hali ya kibinadamu Gaza imefikia kiwango cha janga, ambapo zaidi ya watu 70,000 wameuawa, maelfu kujeruhiwa, na zaidi ya watu milioni 2 kukosa makazi. Aliongeza kuwa katika Ukingo wa Magharibi, zaidi ya watu 1,000 wameuawa tangu mwaka 2023, zaidi ya elfu arobaini kufurushwa, na zaidi ya watu 10,000 kuwekwa kizuizini katika mazingira magumu, huku ukatili wa walowezi haramu ukizidi kushamiri dhidi ya raia wa Palestina.
Alilaani kuendelea kwa ukaliaji, vitendo vya ukatili, unyanyasaji wa wafungwa, na uharibifu mkubwa wa miundombinu, akisisitiza kuwa vitendo hivyo ni uhalifu mkubwa na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na misingi ya kibinadamu.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa UNDP ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa umoja wa mataifa Shigeki Komatsubara, akitoa taarifa kwa niaba ya mfumo mzima wa Umoja wa Mataifa, alisema kuwa miaka miwili ya machafuko imesababisha maelfu ya vifo, njaa, na uharibifu mkubwa Gaza, huku kusitishwa kwa mapigano kukileta matumaini mapya. Alisisitiza umuhimu wa kuheshimu sheria za kimataifa na kuendeleza juhudi za kufikia suluhisho la mataifa mawili kulingana na mipaka ya kabla ya mwaka 1967.
Katika hitimisho lake, Bwana Siam alisema: “Amani ya kweli Mashariki ya Kati haiwezekani bila haki kwa watu wa Palestina.” Aliitaka jumuiya ya kimataifa kuonyesha mshikamano wa dhati, kudai uwajibikaji, na kushinikiza hatua zinazolinda haki za watu wa Palestina.
Sherehe hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani (JMAAT), Alhadi Mussa Salum, pamoja na wadau wengine wengi kutoka taasisi mbalimbali na wananchi wa kawaida.
Palestine Embassy Leads Commemoration of International Day of Solidarity in Dar es Salaam
The Embassy of the State of Palestine in Tanzania led the commemoration of the International Day of Solidarity with the Palestinian People, attended by representatives of the United Nations, members of the Solidarity Committee, members of the Palestinian community, and various invited guests.
Speaking at the event, the Charge d'Affairs of Palestine, Councelour Mr. Salim Siam, stated that since the adoption of UN Resolution 181 in 1947, the rights of the Palestinian people have continued to be violated, while the State of Palestine with its capital Jerusalem remains and brutal Israel Occupation.
Mr. Siam explained that the humanitarian situation in Gaza has reached catastrophic levels, with more than 70,000 people killed, thousands injured, and over 2 million people displaced. He added that in the West Bank, more than 1,000 people have been killed since 2023, with more than fourty thousands displaced, more than 10,000 imprisoned in the hard condition with the escalation of the illegal settlers violance against Palestinian people in the West Bank.
He condemned the continued occupation, violence, mistreatment of detainees, and widespread destruction of infrastructure, stressing that these actions constitute genocidal acts and clear violation of international low and humanitarian principles.
For his part, the UNDP Representative, who also serves as the UN Resident Representative, Shigeki Komatsubara, delivering a statement on behalf of the entire UN system, stated that two years of conflict have resulted in thousands of deaths, widespread hunger, and extensive destruction in Gaza, while the recent ceasefire has brought renewed hope. He emphasized the importance of upholding international law and advancing efforts toward a two-state solution based on the pre-1967 borders.
In his concluding remarks, Mr. Siam stated: “True peace in the Middle East is impossible without justice for the Palestinian people.” He called on the international community to demonstrate genuine solidarity, demand accountability, and push for actions that protect the rights of the Palestinian people.
The ceremony was attended by various participants, including the Chairman of the Reconciliation and Peace Community Committee (JMAAT), Alhadi Mussa Salum, along with other stakeholders from different institutions and members of the general public.







0 Comments