Mwandishi Maalum wa UN: Kwa Nini Mwendesha Mashtaka wa ICC Hajaiomba Hati ya Kukamatwa kwa Smotrich wa Israel?

Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ufwatiliaji wa hali ya haki za binadamu katika Maeneo ya Palestina yaliyokaliwa, Francesca Albanese amesema haelewi kwa nini mpaka sasa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) hajaomba hati ya kukamatwa kwa Waziri wa Fedha wa Israel.

Francesca alimtuhumu Smotrich kuwa mchoraji mkuu wa sera za kimbari za Israel dhidi ya Wapalestina.

Kauli hii ilitolewa baada ya Baraza la Mawaziri la Israel kuidhinisha mpango wa Smotrich, ambao unajumuisha uhalalishaji wa vituo vitano vya makazi huko huko katika Ukingo wa Magharibi (West Bank)

"Hata kwa kuzingatia shinikizo kubwa la kisiasa kwa ICC, sioni kwa nini Mwendesha Mashtaka wa ICC hajaomba hati ya kukamatwa kwa mtu huyu, ambaye ni mchoraji mkuu wa sera za kimbari za Israel dhidi ya Wapalestina," alisema katika chapisho lake  kwenye mtandao wa Twitter (X)

Post a Comment

0 Comments