Waisraeli Mamia Wavamia Msikiti wa Al-Aqsa Chini ya Ulinzi Mkali Kabla ya Maandamano ya "Bendera"

Mamia ya Waisraeli wamevamia Msikiti wa Al-Aqsa, wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi wa Israeli, kabla ya maandamano ya kila mwaka ya "bendera" yanayoendeshwa na watu wa mrengo mkali wa kulia kupitia Jerusalem Mashariki inayokaliwa.

Takriban Waisraeli 800 walivamia msikiti huo Jumatano asubuhi, wakiingia kupitia Lango la Moroko. Wakiwa hapo, walifanya matembezi ya kichokozi kwenye eneo hilo, wakiandamana na marabi na wanasiasa, akiwemo waziri wa Israeli Yitzhak Wasserlauf, mbunge Yitzhak Kreuzer, na Moshe Feiglin, mbunge wa zamani wa mrengo mkali wa kulia.

Maandamano hayo ya bendera, ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Jerusalem inayokumbuka kukaliwa kwa mji huo mwaka 1967, ni gwaride la mrengo mkali wa kulia ambalo lina husishwa na ghasia dhidi ya Wapalestina na "maonyesho ya uchochezi, utawala wa Kiyahudi, na ubaguzi wa rangi," kulingana na NGO ya Israeli Ir Amim.

Zaidi ya maafisa wa usalama wa Israeli 3,000 wamepelekwa Jerusalem Mashariki kwa ajili ya tukio hilo.






Post a Comment

0 Comments