Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina Yapongeza Vikwazo vya Ufaransa kwa Walowezi wa Kiyahudi Wanaodaiwa Kuchochea Vurugu

Wizara ya Mambo ya Nje na Wahamiaji imepokea kwa furaha uamuzi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa wa kuweka vikwazo kwa walowezi 28 wa Kiyahudi wanaodaiwa kuhusika katika mashambulizi na vurugu dhidi ya raia wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi uliokaliwa (WestBank). Wizara Inaona huu ni uamuzi wa kishujaa na hatua muhimu kuelekea ulazima wa kuweka vikwazo zaidi kwa mfumo mzima wa makazi ya walowezi katika ardhi yote ya Nchi ya Palestina.

Wizara inaomba nchi zote kuweka vikwazo vikali, si tu kwa walowezi wanaoendeleza vitendo vya ukatili bali pia kuorodhesha mashirika ya walowezi wenye msimamo mkali kwenye orodha ya ugaidi, pamoja na mfumo mzima wa ukoloni. Wizara Inasisitiza kutumia shinikizo kwa nchi inayokalia ardhi hiyo ili kuilazimisha kusitisha shughuli za makazi, kuvunja vikosi vya wanamgambo wa walowezi wenye silaha, na kuondoa silaha zao.

In English:
Palestinian Foreign Ministry Applauds France's Sanctions on Alleged Jewish Settlers Inciting Violence

The Palestinian Foreign Ministry Applauds France's Sanctions on Alleged Jewish Settlers Inciting Violence and Expatriates welcomes the decision of the French Ministry of Foreign Affairs to impose sanctions on 28 extremist Israeli settlers involved in attacks and violence against Palestinian citizens in the occupied West Bank. It considers this a courageous decision and a significant step in the right direction towards the necessity of imposing more sanctions on the entire colonial settlement system in the entire land of the State of Palestine.

The ministry urges all countries to impose deterrent sanctions not only on extremist settlers but also to place terrorist settler organizations on terrorism lists, along with the entire colonial system. It calls for exerting pressure on the occupying state to compel it to stop settlement activities, dismantle armed settler militias, and withdraw their weapons.

Post a Comment

0 Comments