THEY DESTROY GAZA BY BOMBS GREATER THAN HIROSHIMA

What would happen if we collected all the explosives Israel dropped on Gaza into one bomb and detonated it?

Since the beginning of the Israeli assault on Gaza, the Israeli army has dropped thousands of tons of explosives on the region.
Israel had started intense and continuous shelling on the Gaza Strip since October 7th, following the "Operation Al-Aqsa Tempest" launched by the Palestinian resistance against settlements near Gaza on the same day.

By today (November 2nd), the number of martyrs in Gaza since the start of the Israeli aggression has reached 9,061.
How much explosive material was dropped on Gaza?

The Euro Mediterranean Observatory for Human Rights stated today that Israel has dropped more than 25,000 tons of explosives on the Gaza Strip as part of its large-scale ongoing war since October 7th last year.

The observatory added that Israel deliberately uses a mixture known as "RDX" (Research Department Explosive), which is also referred to as "complete explosive," and its power is equivalent to 1.34 times that of "TNT."

This means that the explosives dropped on Gaza amount to more than 30,000 tons.

More than Hiroshima bombs

It's worth noting that the nuclear bomb dropped by the United States on Hiroshima and Nagasaki in Japan at the end of World War II in August 1945 was estimated to be about 15,000 tons of explosives.
This means that the destructive power of the explosives dropped on Gaza exceeds that of what was dropped on Hiroshima, with the observation that the area of the Japanese city is 900 square kilometers, while the area of Gaza is no more than 360 kilometers, according to the Mediterranean Observatory.



SWAHILI
Swali kubwa ni nini kitatokea tukikusanya milipuko yote iliyorushwa na Israel kuelekea ukanda Gaza kuwa bomu moja?

Tangu kuanza kwa shambulio la Israel dhidi ya Gaza, jeshi la Israel limeirusha tani elfu kadhaa za milipuko kwenye eneo hilo.

Israel ilianza mashambulizi makali na ya mara kwa mara dhidi ya Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7, kufuatia "Operesheni Al-Aqsa Tempest" (Al-Aqsa Storm) iliyoanzishwa na wanaharakati wa Palestina dhidi ya vitongoji vya karibu na Gaza.

Hadi Novemba 2, idadi ya mashahidi (waliofariki) huko Gaza tangu kuanza kwa uvamizi wa Israel imefikia 9,061.

Je ni Kiasi gani cha milipuko kimetupwa Gaza?

Kituo kinachosimamia masuala ya haki za binadamu Euro Mediterranean kimetangaza kuwa Israel imetupa zaidi ya tani 25,000 za milipuko katika Ukanda wa Gaza kama sehemu ya vita vyake kubwa tangu Oktoba 7

Kituo hicho kimeongeza kuwa Israel inatumia kwa makusudi mchanganyiko unaojulikana kama "RDX" (Research Department Explosive), ambao pia unajulikana kama "milipuko kamili," na nguvu yake ni mara 1.34 ya "TNT."

Hii inamaanisha kuwa milipuko iliyorushwa Gaza inazidi tani 30,000. Zaidi ya mabomu ya Hiroshima

Ni muhimu kuzingatia kuwa bomu la nyuklia lililorushwa na Marekani huko Hiroshima na Nagasaki nchini Japan mwishoni mwa Vita vya pili vya dunia mnamo Agosti 1945 lilikadiriwa kuwa na takriban tani 15,000 za milipuko.

Hii ina maana kuwa nguvu ya milipuko iliyotupwa Gaza inazidi ile iliyotupwa Hiroshima, huku ikizingatiwa kuwa eneo la mji huo wa Japani ni kilomita za mraba 900, wakati eneo la Gaza halizidi kilomita za mraba 360.

kulingana na Kituo cha Uangalizi cha Euro Mediterranean.

Post a Comment

0 Comments