Waziri Shahin Afanya Mkutano Mtandaoni na Mabalozi wa Palestina kwa Nchi za Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje na wapalestina waishio nje Varsen Shahin alifanya mkutano wa mtandao na Mabalozi wa Palestina katika nchi za Afrika. Alipongeza jitihada zao za kueleza mateso ya watu wa Palestina na kutetea haki zao katika vikao mbalimbali vya kikanda na kimataifa.

Wakati wa mkutano huo, Waziri alitoa taarifa ya kisiasa ya kina kuhusu maendeleo ya hivi karibuni kwenye eneo la Palestina, na kuwapa mabalozi maelezo kuhusu matokeo ya ziara yake ya hivi karibuni katika nchi tatu za Afrika. Alisisitiza umuhimu wa ziara hiyo katika kuimarisha uwepo wa kisiasa wa Palestina na kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi za Afrika.

Shahin alisisitiza umuhimu wa kujijenga zaidi kutokana na matokeo ya ziara hiyo na kuongeza juhudi za kidiplomasia kwa pamoja na nchi za Afrika, akionyesha nafasi kubwa inayoongezeka na uzito wa kisiasa wa bara hilo katika kusaidia haki za Palestina. Aliwataka mabalozi kuongeza ushirikiano wao kisiasa lakini pia ushirikiano na vyombo vya habari, kupanua wigo wa msaada na kuunga mkono nafasi za taaifa la Palestina kikanda na kimataifa.

......................................................................

Minister Shahin Holds Virtual Meeting with Palestinian Ambassadors to African Countries Minister of Foreign Affairs and Expatriates

Varsen Shahin held a virtual meeting today with the Ambassadors of the State of Palestine to African countries. She commended their efforts in conveying the suffering of the Palestinian people and defending their legitimate rights in various regional and international forums. 

During the meeting, the Minister provided a comprehensive political briefing on the latest developments on the Palestinian scene, and briefed the ambassadors on the outcomes of her recent visit to three African countries. She highlighted the importance of this tour in strengthening Palestine’s political presence and consolidating bilateral relations with African states. 

Shahin emphasized the need to build on the results of the visit and to intensify joint diplomatic efforts with African countries, underscoring the continent’s growing role and political weight in supporting Palestinian rights. She called on the ambassadors to further enhance their political and media engagement, and to broaden the scope of support and endorsement for the positions of the State of Palestine at both the regional and international levels.

Post a Comment

0 Comments